Mada kuu katika toleo hili la tatu la Riziki 2024 ni Mungu wa Agano. Tunakumbushana kuwa upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni upendo wa kipekee ambao hauwezi kulinganishwa na upendo wa aina yoyote ile. Ahadi ya kwamba hatatuacha yafungamana na agano lake nasi… Nikukaribishe kusoma - Bonyeza HAPA
Read More
Katika toleo hili tutajifunza jambo la muhimu sana tunapotaka kumpendeza Mungu na wanadamu. Jambo hili ni UTII. Kutii ni pamoja na swali gumu. Je, nimtii Mungu au mwanadamu? Wewe umewahi kujiuliza hivyo? Karibu kusoma toleo hili. TSH. 500 tu.
Read More
Mada kuu katika toleo hili la pili la Riziki 2024 ni agizo la Yesu, “Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu”. Je, uko tayari kusema, “Niko hapa Bwana, nitume mimi”?
Bonyeza hapa kusoma RIZIKI ONLINE
Read More
Karibu kusoma toleo hili ujifunze zaidi juu ya Yesu rafiki yetu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hili. Tsh. 500 tu.
Read More
Mada kuu katika toleo hili la kwanza la Riziki 2024 ni Yesu Uhai Wetu. Kama vile uhai wa kipepeo ulivyokuwa mikononi mwa mjukuu, ndivyo tunavyokumbushana kuwa uhai wetu uko mikononi mwa Yesu. Aliye na Yesu anao uzima; ambaye hana Yesu, hana huo uzima. Karibu kusoma HAPA bure.
Read More
Nikukaribishe kusoma toleo hili. Linatufundisha kuwa sisi ni zawadi ya Mungu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hilo. Je, unamkumbuka mtoto aliyekuwa na kikapu chenye samaki wawili na mikate mitano? Soma uk.14 uone mtoto huyu alifanya nini akawa baraka ya Mungu kwa maelfu ya watu. Usisahau michezo na katuni kuhusu Dada Rehema na wadogo zake. Karibu Soma Biblia upate nakala kwa Tsh. 500 tu.
Read More
Mada kuu katika toleo hili la nne la Riziki 2023 ni Yesu Kristo ni njia ya uzima. Kuna njia nyingi, lakini tunakumbushana kuwa kuna njia moja tu ya kumwingiza mtu katika furaha ya kweli ya milele. Kuna ukweli mmoja tu umfanyao mtu kuwa huru. Kuna namna moja tu ya maisha itakayomfikisha mtu katika uzima wa milele. Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ndiye Njia hiyo moja.
Read More
Je, mahubiri ya siku ya Siku Kuu ya Watoto yanawalenga akina nani hasa? Ni kwa ajili ya wazazi wanaowalea watoto au ni kwa ajili ya watoto ambao kimsingi ndio wenye siku yao? Mada kuu ya toleo la tatu la Riziki inasema “tuwafundishe watoto wetu“. Lengo la mada hii ni kukumbushana kama familia, kanisa na jamii kuweka mkazo katika malezi ya watoto. “Na watoto wako wote watafundishwa na BWANA; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi” ( Isa 54:13). Karibu kusoma RIZIKI ONLINE BURE. BOFYA HAPA
Read More
Katika toleo hili utaweza kuelewa zaidi upendo wa Yesu kwetu sisi wanadamu. Kupitia makala ya Simulizi kwa mfano utasimuliwa jinsi Yesu alivyokasirika kuona wanafunzi wake wakiwakataza watoto wasiende kwake. Unajua Yesu alifanya nini siku hiyo? Karibu usome! Na usisahau makala nyingine, vibonzo na michezo. Yote yatakupa uelewa zaidi juu ya upendo wa Mungu kwetu.
Bonyeza hapa kupata orodha ya bei ya vitabu mbali mbali na Biblia
Read More
Katika toleo la pili la gazeti la Riziki tunajadiliana kichwa kisemacho, Vijana wanaandaliwaje kabla ya ndoa? Lengo la mada hii ni kuchochea na kuamsha mjadala juu ya kuandaa vijana wanaotarajiwa kuingia katika ndoa katika misingi ile aliyoiweka Mungu ili hata ndoa zao zitakapopata mitikisiko, bado waweze kusimama katika kumtegemea Mungu.
Soma RIZIKI ONLINE HAPA
Read More
Katika toleo hili la Riziki tunajadili kichwa kisemacho, “Kuishi maisha ya ushuhuda’’. Lengo ni kukumbushana kuwa kila mmoja wetu anayo hadithi ya kushuhudia. Hadithi yako kuhusu kutembea na Kristo au changamoto ulizokutana nazo maishani zinaweza kufundisha, kujenga na kubadilisha maisha ya mtu mwingine anayepita kwenye hali kama yako.
Bonyeza hapa kusoma bure - RIZIKI ONLINE
Read More
Maombi yanamkaribisha Yesu ndani yetu. Yanatupa nafasi ya kuzungumza na Mungu kwa karibu zaidi – kama mtoto anavyoongea na baba mzazi anayempenda. Maombi yanajibiwa kwa mapenzi ya Mungu kwetu. Mungu anatupenda, na anatukaribisha tumwombe lolote tutakalo naye atatupa. Basi ukiwa na jambo lolote, nenda katika maombi umweleze Mungu naye atajibu.
Karibu usome toleo hili linalofafanua zaidi juu ya kujibiwa maombi. Linauzwa Tsh. 500 tu, katika Maduka ya Soma Biblia
Read More
Bwana Yesu Asifiwe!
Karibu kununua Twende katika maduka ya Soma Biblia.
Katika toleo hili tutajifunza juu ya Likizo na mapumziko.
Read More
Katika toleo hili tutajifunza juu ya msamaha.
TWENDE ni gazeti la Kikristo kwa Watoto na Vijana. Kupitia gazeti hili, tunataka kufundisha Watoto na vijana Injili ya uzima wa milele ndani ya Yesu Kristo. TWENDE inatolewa mara nne kwa mwaka. Bei: 500 Tsh kwa nakala moja. Karibu dukani Soma Biblia
Read More
Toleo hili la Riziki linaongozwa na mada isemayo “Tumeitwa kutenda mema”. Msingi wa mada hii unatokana na ukweli kwamba tunaishi katika nyakati ambazo ukatili na kutokuthaminiana kumekuwa kwa kiwango cha juu sana. Lakini pia majadiliano yanaenda zaidi, maana kutenda mema peke yake hakutoshi kama una tarajio la kuurithi uzima wa milele.
Bonyeza HAPA kusoma bure
Read More
Katika toleo hili la Riziki tunajadili mada isemayo, Je, Mungu anaweza kumwacha mwanadamu? Msingi wa swali hili unatokana na hali ambazo tunakutana nazo kwenye maisha. Kuna wakati unapita mahali pagumu na kufikia hatua ya kufikiri kwamba Mungu amekuacha. Bila shaka, wakati wa shida na uhitaji mkuu ungetamani kuona mtu unayehusiana naye vyema akiwa karibu nawe kukutia moyo na kukusaidia. Vipi usipomwona, unajisikiaje?
Karibu kusoma zaidi Hapa bure
Read More
Katika toleo hili tunajifunza juu ya 'Kukaza Mwendo'. Kupitia makala mbalimbali tutajifunza maana hasa ya kukaza mwendo kwenda Mbinguni, na zaidi tuta-elewa kuwa sisi ni washindi tunaoweza kuzishinda changamoto za dunia hii kwa sababu yupo mmoja ambaye anatuwezesha kushinda tukiwa naye.
Kuna kibonzo kitakachokufurahisha na kukufundisha kukaza mwendo bila kukata tamaa hadi kufikia ushindi. Usisahau dada Rehema! Ana michezo na ukijibu maswali vizuri unapata zawadi. Pia Kaka Kalamu anakukumbusha kumwandikia kama una swali, naye atakujibu. Karibu tusome!
Read More
Nina mashaka, nifanye nini?
Tunapoelekea sehemu ya mbali na ni mara ya kwanza kupita katika njia ile, tunakuwa makini tusipotee. Hali ya safari inakuwa na changamoto zaidi pale tunapokutana na njia zaidi ya moja. Je, tufuate njia ipi?
Ndani yetu kunaweza kujengeka mashaka kuwa tupo karibu na kupotea. Lakini tunapopata kuelewa na kuifuata njia iliyo sahihi, tunapata tena furaha ya safari.
Mtoto mwenzangu, jambo hili hutokea pia katika safari yetu ya imani. Wakati mwingine changamoto ikitukuta njiani, tumaini letu linapotea, na tunapata woga na wasiwasi mkubwa. Je, tufanye nini?
Yesu anatuambia, 'Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha' (Mathayo 11:28). Yesu anaweza kutuondolea mashaka yote tuliyonayo. Unajua anafanyaje?
Toleo hili linafafanua jinsi kuu ya kuondokana na mashaka, nayo ni kumfuata Yesu. Yeye ni Mungu pamoja nasi. Kupitia makala mbalimbali, michezo na katuni, utajifunza na kuelewa zaidi habari hii njema.
Karibu kununua dukani Soma Biblia kwa 500/= tu.
Katika toleo hili la kwanza la Riziki kwa mwaka huu 2022, tunajadili masuala ya kipindi cha Kwaresima. Kanisa na waumini wake hufanya nini, na kwa nini? Na je, njia ipi ni bora zaidi, ukitaka kutumia vema kipindi hiki cha siku 40 kabla ya Pasaka?
Utakutana na kijana mmoja ambaye alitoa wito wa ajabu kwa wanafunzi wenzake akiwaambia, “Twendeni nasi tukafe naye” (yaani, Yesu).
Utapata pia makala mbalimbali za kukujenga na kukuimarisha kiroho, na kukusogeza karibu na Mungu. Katika majira haya ya Kwaresima naungana na nabii Yoeli kwa maneno haya, “Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya” (Yoe 3:13).
SOMA BURE HAPA, RIZIKI
Katika toleo hili la Riziki tunajadili kuhusu nguvu ya msalaba. Ni mahali ambapo Yesu Kristo alitundikwa yapata miaka elfu mbili iliyopita, lakini tukio lile lilisababisha mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu. Ni tukio hili ambalo lilirudisha uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Yeye ambaye hapo kwanza alikuwa amegombana na Baba yake wa mbinguni, sasa amerudishiwa nafasi yake kama mtoto na mrithi pamoja na Kristo.
Read More