Contact Us

Use the form on the right to contact us.

Or use the information below to contact our main office in Dar es Salaam or Arusha.

Main office:

P.o. box 12772 Dar Es Salaam, Tanzania

Phone: +255 686 313 721 or +255 744 339 167

E-mail: manager.somabiblia@gmail.com

Publishing department

Postal address: P.o. Box 2696 Arusha, Tanzania

Phone: + 255 787392951

E-mail: publishingmanager.somabiblia@gmail.com

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

RIZIKI 2, 2023 - FINAL PRINT-1.jpg

RIZIKI

RIZIKI ni gazeti la Kikristo linalotolewa mara nne kwa mwaka. Gazeti hili limewalenga Wainjilisti na Wachungaji, lakini pia ni nzuri kwa wote wanaotafuta mafundisho mazuri katika maisha yao ndani ya kristo.

Lengo kuu la RIZIKI ni kuhamasisha na kufundisha wote wanaopeleka neno kwa watu, na kufikisha neno kwa usahihi wote ili kuwajenga watu.

Kujiunga na RIZIKI, tafadhali jaza fomu hapo kulia, au wasiliana nasi kupitia simu au barua, na tutakufikia popote ulipo.

RIZIKI Soma Biblia, 0759 544 917, S.L.P. 2696 Arusha, Tanzania

RIZIKI is the Swahili word used in The Lords prayer for "daily bread". And is the name for Soma Biblia's magazine for Swahili speaking pastors and evangelists. 

Being a servant of the church can be exhausting. And many work in remote areas, with small or no means of inspiration or enlightenment. The main goals of RIZIKI is to encourage and enlighten those who are bringing the word to the people, and present the Word in a holistic way.

RIZIKI comes out four times a year and is distributed for free.  To subscribe to RIZIKI, please fill in the form, and we will get in touch with you.

Riziki #2,2022

Katika toleo hili la Riziki tunajadili mada isemayo, Je, Mungu anaweza kumwacha mwanadamu? Msingi wa swali hili unatokana na hali ambazo tunakutana nazo kwenye maisha. Kuna wakati unapita mahali pagumu na kufikia hatua ya kufikiri kwamba Mungu amekuacha. Bila shaka, wakati wa shida na uhitaji mkuu ungetamani kuona mtu unayehusiana naye vyema akiwa karibu nawe kukutia moyo na kukusaidia. Vipi usipomwona, unajisikiaje?

Bonyeza Hapa kusoma bure online

RIZIKI #3, 2021

RIZIKI #3, 2021

Ufafanuzi wa Sala ya Bwana umefikia tamati katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya kumsifu Mungu tukikiri, “Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina”.

Bonyeza HAPA kusoma RIZIKI online bure

RIZIKI 2, 2020 web cover.jpg

RIZIKI #2, 2020

Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna tunavyo-weza kufikia maisha kwa kuandaa viongozi walio bora kuanzia katika umri wa ujana. Nia ni kuliamsha kanisa kama taasisi muhimu na ya kuaminika katika kuandaa viongozi wenye hofu ya Mungu, wenye maadili mema, wachapa kazi na walio tayari kuacha maslahi yao kwa ajili ya wengine.

Soma Riziki Online HAPA

Riziki 3, 2019, cover.jpg

RIZIKI #3, 2019

Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna ya kutambua nafasi ya watoto na vijana ndani ya kanisa. Nia ni kukumbushana kama kanisa umuhimu wa kuwatambua, ili tuwalee vizuri na kuwajali pamoja na vipaji walivyo navyo.

Soma Riziki Online Hapa

RIZIKI  4, 2018 Final print-1.jpg

RIZIKI #4, 2018

Katika toleo hili la RIZIKI tunaangalia sehemu ya tatu ya Imani ya Mitume inayoanza kwa kusema, Namwamini Roho Mtakatifu.

Karibu kusoma RIZIKI online hapa

RIZIKI  1 2018_cover.jpg

RIZIKI # 1, 2018

Katika RIZIKI toleo la kwanza, 2018, tutasoma na tafakari Yuda 1:3. Je, nini itatokea kwa imani yetu, ikiwa kila kizazi huibadilisha tu kulingarna na mawazo, mahitaji na mipango yake?

Soma RIZIKI toleo #1, 2018 hapa

RIZIKI #1,2022

Katika toleo hili la kwanza la Riziki kwa mwaka huu 2022, tunajadili masuala ya kipindi cha Kwaresima. Kanisa na waumini wake hufanya nini, na kwa nini? Na je, njia ipi ni bora zaidi, ukitaka kutumia vema kipindi hiki cha siku 40 kabla ya Pasaka? 

Bonyeza hapa kusoma bure, RIZIKI

RIZIKI #2,2021Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya nne, Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Ndani ya toleo hili utakutana na watu waliopita katika majaribu yaliyogusa kila eneo la maisha yao. Hata hivyo walisimama katika imani, na hatimaye walitoka wakiwa kama dhahabu safi ing’aayo. Siri yao ikoje? Soma makala za toleo hili, na ujifunze – kwa ajili ya maisha yako mwenyewe ili uweze kuwasaidia vema wanaojaribiwa!

RIZIKI #2,2021

Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya nne, Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Ndani ya toleo hili utakutana na watu waliopita katika majaribu yaliyogusa kila eneo la maisha yao. Hata hivyo walisimama katika imani, na hatimaye walitoka wakiwa kama dhahabu safi ing’aayo. Siri yao ikoje? Soma makala za toleo hili, na ujifunze – kwa ajili ya maisha yako mwenyewe ili uweze kuwasaidia vema wanaojaribiwa!

RIZIKI 1, 2020 - Ypu version -1.jpg

RIZIKI #1, 2020

Katika toleo hili la RIZIKI tunaangalia mada isemayo, “Ujenzi wa familia imara”. Lengo ni kuibua na kujadili changamoto zilizopo kwenye taasisi hii muhimu ambayo mwanzilishi wake ni Mungu mwenyewe pale bustani ya Edeni. Ni wito wa kuliamsha kanisa na jamii yote, kuwa taasisi hii inapaswa kulindwa, kuimarishwa na kupiganiwa kwa nguvu zote.

Kusoma Riziki Bonyeza HAPA

Riziki 2, 2019. final print (BLEED)-1.jpg

RIZIKI #2, 2019

Katika toleo hili la Riziki tunajadili kuhusu umisioni wa ndani. Lengo ni kukumbusha juu ya Utume mkuu wa Bwana Yesu wa kwenda kuhubiri habari njema ya toba na ondoleo la dhambi kwa wale ambao hawajafikiwa na injili.

Soma Riziki Online hapa

RIZIKI  3, 2018 final print-1.jpg

RIZIKI #3, 2018

Toleo hili la 3 la RIZIKI tunaangalia sehemu ya pili ya Imani ya Mitume; Namwamini Yesu Kristo. Tunakumbushana kwa kutafakari maana ya maneno haya.

Soma RIZIKI toleo #3, 2018 hapa

RIZIKI  4 2017 final jpeg_Page_1.jpg

RIZIKI # 4, 2017

Ushindi katika mpango wa Mungu hautegemei maendeleo, mafanikio, pesa, mali, akili, uwezo au chochote tulicho nacho. Ushindi wa Mungu ndio kwamba Yesu aliishinda mauti; na kwa sababu Mungu anatupenda ndiye "atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo" (1 Kor 15:57).

Soma RIZIKI tole #4, 2018 hapa

RIZIKI 3, 2020 issues-1.jpg

RIZIKI #3, 2020

Katika toleo hili la RIZIKI tunaanza na mfululizo wa makala kuhusu Sala Kuu au Sala ya Bwana. Sala hii ina-tufundisha kuwa sifa zote, heshima na utukufu ni kwa Mungu wetu peke yake. Kazi yetu katika maisha ya hapa duniani na hata kifoni ni kumletea Mungu utukufu kwa kila tufanyalo. Sala hii ambayo unaweza kuiomba chini ya dakika moja inatuonyesha ukuu, urefu, upana na kina cha upendo wa Mungu kwetu kupitia Yesu Kristo. 

Soma Riziki Online hapa

RIZIKI 1, 2021 web-1.jpg

RIZIKI #1, 2021

Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya tatu, Utusamehe makosa yetu, kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea. Msamaha ni jambo lenye nguvu sana. Tunapenda sana msamaha, lakini mara nyingi tunapotakiwa kukiri makosa yetu au kuwasamehe waliotukosea, tunaliona kuwa jambo gumu. Tunapenda kupokea msamaha lakini hatupendi kuutoa

Kusoma Riziki Bonyeza HAPA

RIZIKI #4,2021

Katika toleo hili la Riziki tunajadili kuhusu nguvu ya msalaba. Ni mahali ambapo Yesu Kristo alitundikwa yapata miaka elfu mbili iliyopita, lakini tukio lile lilisababisha mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu. Ni tukio hili ambalo lilirudisha uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Yeye ambaye hapo kwanza alikuwa amegombana na Baba yake wa mbinguni, sasa amerudishiwa nafasi yake kama mtoto na mrithi pamoja na Kristo. 

Soma HAPA bure

RIZIKI 4, 2020 issue-1.jpg

RIZIKI #4, 2020

Toleo hili la RIZIKI ni muendelezo wa kuangalia Sala ya Bwana, sehemu ya pili isemayo “Utupe leo riziki yetu”. Sehemu hii inatufundisha kumwendea Mungu kwa moyo wa unyenyekevu na kumtegemea, tukimwomba atupe riziki yetu ya kila siku. Tunatiwa moyo tupeleke mahitaji yetu yafahamike kwa Mungu, tukiamini kuwa tutapewa. Kwa kuomba hivi tunakubali kwamba, kila tunachohitaji kwa ajili ya maisha yetu ya leo ni zawadi kutoka kwa Mungu. 

Soma Riziki Online hapa

Riziki 4, 2019 final-1.jpg

RIZIKI #4, 2019

Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili kurudi kwa Yesu kama alivyoahidi. Lengo ni kusaidiana kama kanisa kupeana maarifa yenye uhakika juu ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Malengo ni wazi: Kwanza, tuwe na mafundisho sahihi kuhusu kurudi kwa Yesu. Pili, tuepukane na mafundisho ya uongo kuhusu jambo hili. Na tatu, tusije tukakata tamaa kuwa Kristo harudi, kisha tukalegea katika kuitenda kazi ya Mungu.

Kusoma Riziki Bonyeza HAPA

RIZIKI  1, 2019 final print-1.jpg

RIZIKI #1, 2019

Katika toleo hili la RIZIKI tunachunguza kama Ukristo ni imani au utamaduni. Nia ni kukumbushana kuwa, mapokeo ya dini yanaweza kuwa mazoea au taratibu tupu zisizo na faida. Kama mwandishi mmoja alivyoandika, ndivyo taratibu zilivyo kama misingi yake haikujengwa katika Kristo. Lakini vilevile tamaduni na mapokeo zitafaa, tena zitakuwa na faida, kama zinatuelekeza kumwamini Yesu na kufanya mapenzi yake.

Soma RIZIKI Online hapa

RIZIKI  2, 2018 print final.jpg

RIZIKI # 2, 2018

RIZIKI toleo la pili, 2018 linaweka fokasi kwenye sehemu ya kwanza ya Imani ya Mitume: Namwamini Mungu, Baba mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi. Kwa mfano ina maana gani kwamba Mungu ni Baba mwenyezi?

Soma RIZIKI toleo #2, 2018 hapa