Mada kuu katika toleo hili la nne la Riziki 2024 inasema, Katika bonde bado Mungu yupo? Ni swali ambalo ni muhimu kutafakari ili tuwatie moyo wale ambao wanapita katika hali ngumu na kukata tamaa. Ni msaada kwa wale ambao wanapita na watakaopita katika bonde la uvuli wa mauti na kuogopa kuwa hakuna tumaini tena kwa maisha ya mbele.
Read More
Mada kuu katika toleo hili la kwanza la Riziki 2024 ni Yesu Uhai Wetu. Kama vile uhai wa kipepeo ulivyokuwa mikononi mwa mjukuu, ndivyo tunavyokumbushana kuwa uhai wetu uko mikononi mwa Yesu. Aliye na Yesu anao uzima; ambaye hana Yesu, hana huo uzima. Karibu kusoma HAPA bure.
Read More
Katika toleo la pili la gazeti la Riziki tunajadiliana kichwa kisemacho, Vijana wanaandaliwaje kabla ya ndoa? Lengo la mada hii ni kuchochea na kuamsha mjadala juu ya kuandaa vijana wanaotarajiwa kuingia katika ndoa katika misingi ile aliyoiweka Mungu ili hata ndoa zao zitakapopata mitikisiko, bado waweze kusimama katika kumtegemea Mungu.
Soma RIZIKI ONLINE HAPA
Read More
Katika toleo hili la Riziki tunajadili mada isemayo, Je, Mungu anaweza kumwacha mwanadamu? Msingi wa swali hili unatokana na hali ambazo tunakutana nazo kwenye maisha. Kuna wakati unapita mahali pagumu na kufikia hatua ya kufikiri kwamba Mungu amekuacha. Bila shaka, wakati wa shida na uhitaji mkuu ungetamani kuona mtu unayehusiana naye vyema akiwa karibu nawe kukutia moyo na kukusaidia. Vipi usipomwona, unajisikiaje?
Karibu kusoma zaidi Hapa bure
Read More
Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya nne, Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Mikononi mwa Mu-ngu majaribu yanaweza kuimarisha imani yetu na kutupa uzoefu kwamba Mungu ni mwaminifu na mwenye uwezo wa kutupitisha salama kiroho. Tunapopatwa na majaribu, kisha tukavuka salama, imani yetu huwa inaongezeka. Yesu anatuombea kila wakati; tulindwe na yule mwovu. Lengo la ombi hili ni kwamba, hata katikati ya majaribu, tulindwe dhidi ya hila za yule mwovu na tuvuke salama.
Ndani ya toleo hili utakutana na watu waliopita katika majaribu yaliyogusa kila eneo la maisha yao. Hata hivyo walisimama katika imani, na hatimaye walitoka wakiwa kama dhahabu safi ing’aayo. Siri yao ikoje? Soma makala za toleo hili, na ujifunze – kwa ajili ya maisha yako mwenyewe ili uweze kuwasaidia vema wanaojaribiwa!
Read More
Toleo hili la RIZIKI ni muendelezo wa kuangalia Sala ya Bwana, sehemu ya pili isemayo “Utupe leo riziki yetu”. Sehemu hii inatufundisha kumwendea Mungu kwa moyo wa unyenyekevu na kumtegemea, tukimwomba atupe riziki yetu ya kila siku. Tunatiwa moyo tupeleke mahitaji yetu yafahamike kwa Mungu, tukiamini kuwa tutapewa. Kwa kuomba hivi tunakubali kwamba, kila tunachohitaji kwa ajili ya maisha yetu ya leo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Read More
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna tunavyoweza kufikia maisha kwa kuandaa viongozi walio bora kuanzia katika umri wa ujana. Nia ni kuliamsha kanisa kama taasisi muhimu na ya kuaminika katika kuandaa viongozi wenye hofu ya Mungu, wenye maadili mema, wachapa kazi na walio tayari kuacha maslahi yao kwa ajili ya wengine.
Read More
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili kurudi kwa Yesu kama alivyoahidi. Lengo ni kusaidiana kama kanisa kupeana maarifa yenye uhakika juu ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Malengo ni wazi: Kwanza, tuwe na mafundisho sahihi kuhusu kurudi kwa Yesu. Pili, tuepukane na mafundisho ya uongo kuhusu jambo hili. Na tatu, tusije tukakata tamaa kuwa Kristo harudi, kisha tukalegea katika kuitenda kazi ya Mungu.
Read More
Je, wewe ni mtumishi wa Kanisa? Riziki toleo la Tatu mwaka 2019 linapatikana sasa.
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna ya kutambua nafasi ya watoto na vijana ndani ya kanisa. Nia ni kukumbushana kama kanisa umuhimu wa kuwatambua, ili tuwalee vizuri na kuwajali pamoja na vipaji walivyo navyo.
Read More
Katika toleo hili la Riziki tunajadili kuhusu umisioni wa ndani. Lengo ni kukumbusha juu ya Utume mkuu wa Bwana Yesu wa kwenda kuhubiri habari njema ya toba na ondoleo la dhambi kwa wale ambao hawajafikiwa na injili.
Read More
Katika toleo hili la RIZIKI tunachunguza kama Ukristo ni imani au utamaduni. Nia ni kukumbushana kuwa, mapokeo ya dini yanaweza kuwa mazoea au taratibu tupu zisizo na faida. Kama mwandishi mmoja alivyoandika, ndivyo taratibu zilivyo kama misingi yake haikujengwa katika Kristo. Lakini vilevile tamaduni na mapokeo zitafaa, tena zitakuwa na faida, kama zinatuelekeza kumwamini Yesu na kufanya mapenzi yake. Karibu usome toleo hili
Read More