Karibu Soma Biblia
Ni sawa kabisa kuyaita majengo yetu makubwa na mazuri kanisa. Maana yake ni mahali pa kuabudia. Katika toleo hili tutaagalia maana nyingine ya Kanisa, herufi K ikiwa kubwa. Kanisa hili si jengo bali ni sisi tunaomwamini Yesu Kristo. Ndiyo maana tunasema, "Sisi ni Kanisa la Mungu".
Mada kuu katika toleo hili la nne la Riziki 2024 inasema, Katika bonde bado Mungu yupo? Ni swali ambalo ni muhimu kutafakari ili tuwatie moyo wale ambao wanapita katika hali ngumu na kukata tamaa. Ni msaada kwa wale ambao wanapita na watakaopita katika bonde la uvuli wa mauti na kuogopa kuwa hakuna tumaini tena kwa maisha ya mbele.
Mada kuu katika toleo hili la tatu la Riziki 2024 ni Mungu wa Agano. Tunakumbushana kuwa upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni upendo wa kipekee ambao hauwezi kulinganishwa na upendo wa aina yoyote ile. Ahadi ya kwamba hatatuacha yafungamana na agano lake nasi… Nikukaribishe kusoma - Bonyeza HAPA
Katika toleo hili tutajifunza jambo la muhimu sana tunapotaka kumpendeza Mungu na wanadamu. Jambo hili ni UTII. Kutii ni pamoja na swali gumu. Je, nimtii Mungu au mwanadamu? Wewe umewahi kujiuliza hivyo? Karibu kusoma toleo hili. TSH. 500 tu.
Mada kuu katika toleo hili la pili la Riziki 2024 ni agizo la Yesu, “Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu”. Je, uko tayari kusema, “Niko hapa Bwana, nitume mimi”?
Bonyeza hapa kusoma RIZIKI ONLINE
Karibu kusoma toleo hili ujifunze zaidi juu ya Yesu rafiki yetu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hili. Tsh. 500 tu.
Je, unapenda kuisoma Biblia na kuwa na hamu ya kujifunza zaidi? Basi, unaalikwa kujiunga na Ushirika wa Kujifunza Biblia! Jipatie kitabu kipya kiitwacho Mafunzo ya Biblia. Injili alivyoiandika Mathayo. Kinapatikana Soma Biblia
Bonyeza HAPA kupata bei na orodha ya vitabu vingine
Mfalme anaweza kuwa mzuri au mbaya. Akiwa mfalme mzuri anaonyesha upendo kwa watu wake, na hukumu zake ni za haki. Mfalme mbaya anafikiri juu ya maendeleo yake tu, na hana rehema kwa watu wake. Karibu kusoma toleo hili ujifunze zaidi juu ya Yesu, Mfalme wa wafalme.
Mada kuu katika toleo hili la kwanza la Riziki 2024 ni Yesu Uhai Wetu. Kama vile uhai wa kipepeo ulivyokuwa mikononi mwa mjukuu, ndivyo tunavyokumbushana kuwa uhai wetu uko mikononi mwa Yesu. Aliye na Yesu anao uzima; ambaye hana Yesu, hana huo uzima. Karibu kusoma HAPA bure.
Unatafuta nguvu mpya ya kiroho? Mwongozo huu utakusaidia kujisomea Biblia kwa mpango kila siku mwaka mzima wa 2024. Bado vinapatikana Katika maduka ya Soma Biblia, karibu usichelewe kupata nakala yako
SOMA BIBLIA Society ni shirika la wahisani lisilo la kutengeneza faida wala kuwa na mwelekeo wa kisiasa. Lengo letu kuu ni kusambaza Injili ya Yesu Kristo kwa Kiswahili, kwa kuandaa Kanisa kupitia kuendeleza, kuzalisha na kusambaza Biblia kwa njia ya sauti, machapisho ya kuaminika juu ya Injili na vifaa vingine, vyote kwa Kiswahili. Shabaha nyingine ni kuwasaidia Wakristo kufikisha Injili kwa watu na kuwafundisha kupitia neno la Mungu – juu ya imani na maisha.
Idara ya Uchapishaji
Kama ukiwa na mswada au kutaka Soma Biblia kusambaza kitabu chako. Pia masuala ya Riziki, Twende, na Soma Biblia kwa Njia ya Mtandao
Simu: +255 787 392 951
Barua Pepe: publishingmanager.somabiblia@gmail.com
Anuani ya Posta: S.L.P. 2696, Arusha, Tanzania
Makao: Eneo la Sakina, upande wa pili wa sheli ya mafuta ya Oryx (kituo cha basi huitwa Oil Com). Fuata kibao cha Scripture Mission.
Idara ya Mauzo
Kama ukitafuta kitabu na bei yake, au kutaka kuagiza na kununua vitabu
Simu: +255 754 292 995
Baruapepe: manager.somabiblia@gmail.com
Anuani ya Posta: S.L.P. 12772, Dar es Salaam, Tanzania
Makao: Barabara ya Mwai Kibaki, Mikocheni B, upande wa pili wa Sanitas Medical Centre
Maduka yanapatikana Dar es Salaam (Mikocheni B & Mbezi Luis), Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma na Iringa