Mada kuu katika toleo hili la kwanza la Riziki 2024 ni Yesu Uhai Wetu. Kama vile uhai wa kipepeo ulivyokuwa mikononi mwa mjukuu, ndivyo tunavyokumbushana kuwa uhai wetu uko mikononi mwa Yesu. Aliye na Yesu anao uzima; ambaye hana Yesu, hana huo uzima. Karibu kusoma HAPA bure.
Read More
Mada kuu katika toleo hili la nne la Riziki 2023 ni Yesu Kristo ni njia ya uzima. Kuna njia nyingi, lakini tunakumbushana kuwa kuna njia moja tu ya kumwingiza mtu katika furaha ya kweli ya milele. Kuna ukweli mmoja tu umfanyao mtu kuwa huru. Kuna namna moja tu ya maisha itakayomfikisha mtu katika uzima wa milele. Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ndiye Njia hiyo moja.
Read More
Maombi yanamkaribisha Yesu ndani yetu. Yanatupa nafasi ya kuzungumza na Mungu kwa karibu zaidi – kama mtoto anavyoongea na baba mzazi anayempenda. Maombi yanajibiwa kwa mapenzi ya Mungu kwetu. Mungu anatupenda, na anatukaribisha tumwombe lolote tutakalo naye atatupa. Basi ukiwa na jambo lolote, nenda katika maombi umweleze Mungu naye atajibu.
Karibu usome toleo hili linalofafanua zaidi juu ya kujibiwa maombi. Linauzwa Tsh. 500 tu, katika Maduka ya Soma Biblia
Read More
Katika toleo hili tutajifunza juu ya sauti ya Mungu. Je, unajua Mungu anatuita, na jinsi tunavyoweza kuisikia sauti yake na kuifuata? Karibu kusoma toleo hili uelewe vizuri zaidi.
Read More
Soma Biblia tuna mradi mpya wa kufikisha Injili kwa vijana kupitia kijitabu kinachoitwa Masiha. Kwa njia ya vibonzo, kijitabu hicho kinasimulia habari za Agano Jipya kuhusu maisha ya Yesu hapa duniani tangu kuzaliwa kwake mpaka alipopaa Mbinguni. Ni pamoja na mafundisho yake, na kusulubiwa, kufa na kufufuka kwake.
Read More