SOMABIBLIA KWA NJIA YA MTANDAO
somabiblia kwa njia ya mtandao ni huduma kwa wote wanaotaka kusoma vitabu vyetu kwa manufaa zaidi.
Hii ni huduma kwa wote wanaotaka kusoma vitabu vyetu kwa manufaa zaidi. Vitabu vilivyoorodheshwa katika ukurasa huu, vimeandaliwa kama kozi yenye maswali. Ukiwa mwanafunzi wetu, mwalimu yuko tayari kukushauri, kusahihisha majibu yako na kutoa maoni na maelezo zaidi kwa lengo la kupanua uelewa wako wa mambo unayoyasoma.
Wote wanaofanya vizuri watapokea cheti kinachothibitisha kwamba wamesoma na kuelewa ujumbe wa kitabu kinachohusika. Mafunzo ni bure. Gharama ya kusoma ni bei ya kitabu tu. Vitabu vyaweza kununuliwa madukani kwetu, kwa wasambazaji wetu nchini kote, au kwa kuviagiza kwa somabiblia kwa njia ya mtandao, S.L.P. 2696, Arusha.
Baada ya kujiunga na kuchagua kitabu, mwanafunzi atapokea maswali yake kwa njia ya baruapepe au Posta, kama anavyoamua yeye. Majibu atayatuma kwa ofisi yetu mjini Arusha ambapo yatasahihishwa. Halafu tutamrudishia mwanafunzi majibu yake pamoja na cheti, ikiwa amefaulu vizuri.
Ukitaka kujiunga, peleka barua yenye jina lako, anwani yako na namba ya simu kwa anwani ya hapo juu, au tuma baruapepe kwenda kwa: njiayaposta.somabiblia@gmail.com au piga simu: +255 686 212 165
Au jaza fomu ya kujiunga hapo chini:
Vitabu vya kozi vipo vifuatavyo:
- Dini na Maisha
- Ubatizo wa Kikristo
- Imani Yangu
- Roho Mtakatifu
- Maombi
- Historia ya Kibiblia
- Onjeni Bwana Alivyo Mwema
- Biblia Ijieleze Yenyewe
- Wokovu – Maana na Matokeo
- Al-Kitab
- Israeli kwa Mtazamo wa Kikristo
- Mwongozo kwa Familia ya Kikristo I
- Mwongozo kwa Familia ya Kikristo II