Contact Us

Use the form on the right to contact us.

Or use the information below to contact our main office in Dar es Salaam or Arusha.

Main office:

P.o. box 12772 Dar Es Salaam, Tanzania

Phone: +255 686 313 721 or +255 744 339 167

E-mail: manager.somabiblia@gmail.com

Publishing department

Postal address: P.o. Box 2696 Arusha, Tanzania

Phone: + 255 787392951

E-mail: publishingmanager.somabiblia@gmail.com

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

MIMI NI MKRISTO

Kuwa Mkristo ni kubatizwa na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Je, ni hivyo tu? Kupitia mahojiano na watu mbali mbali tutajifunza kutoka kwao, waliwezaje kuwa Wakristo na kudumu katika Imani na Wokovu wake Yesu Kristo. Utajifunza kupitia ushuhuda wao na jinsi wanavyoishi maisha ya Kikristo.

Ushuhuda wa James Sabuni 'Maongozo ya Mungu ni sahihi kuliko yale ya Wanadamu'

Cathbert Msemo

Karibu kusikiliza ushuhuda wa James Sabuni. Mstari huu wa Biblia anaupenda na ametushirikisha sisi sote tunaosikiliza ushuhuda wake. ‘Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake’ Zaburi 27:4

Read More

Ushuhuda wa Raphael Paul Kallaghe

Cathbert Msemo

Bwana akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo. Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake. Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia; (akaunyosha mkono wake akamshika, naye akageuka kuwa fimbo mkononi mwake;)

Nilikuwa sijui Neno la Mungu hivyo niliona kama nimepotoka na nikavutwa na kwenda upande mwingine. Namshukuru Mungu mama yangu mdogo alikuja na kunishuhudia akisema nilikuwa huko miaka mingi lakini nimeijua kweli na kweli ni Kristo na akanipeleke katika mkutano wa Injili. Napenda Neno hili la Kutoka 4:2-4 na nalitumia kufundisha vijana. Huu ni ushuhuda wa Raphael Paul Kallaghe mfanyakazi wa Soma Biblia Arusha. Ameeleza mengi ya maisha yake ya kuwa Mkristo. Karibu usikilize

Raphael Kallage 2.jpg

Ushuhuda wa John Zakaria Mislay

Cathbert Msemo

Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. ...

Niliumwa sana na hospitali hawakuweza kuona ugonjwa wowote waliponipima, lakini nilimuomba Mungu na akaniponya. Hii mistari ya Zaburi 23:1-6 ina maana sana katika maisha yangu. Mimi inanifariji sana. Ukiwa na Yesu katika maisha yako hutapungukiwa na kitu chochote. Namshukuru Mungu maana sikukata tamaa bali nilimtegemea yeye. Karibu kusikiliza ushuhuda huu kutoka kwa John Zakaria Mislay mfanyakazi wa Soma Biblia Arusha.

John Zakaia.jpg

Joseph Nyngasa Mganga 'Ninamwamini na kumtegemea Yesu Kila wakati'

Cathbert Msemo

Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.

Kupitia neno hili, 2 Timotheo 1:12 nimejifunza kuwa katika maisha ya Imani kuna mateso, lakini ninachotakiwa kufanya ni kumwamini Yesu na kuendelea kumtegemea yeye kila wakati. Karibu kusikiliza ushuhuda wa maisha ya kikristo ya Joseph Nyangasa mfanyakazi wa Soma Biblia.

Joseph Nyangara (2).jpg

Maisha ya Ebenezer Nelson Shafuri 'Mtu asiudharau Ujana wako'

Cathbert Msemo

Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Nilitafakari kupitia mstari huu wa 1 Timotheo 4:12 nikagundua kuwa kwa makundi niliyokuwa nayo ujana wangu ulikuwa unadharaulika. Lakini ukiwa na Yesu na kuacha baadhi ya mambo yasiyopendeza basi hakuna atakayekudharau. Ebenezer anasema haikuwa rahisi kwa wenzake kuelewa maisha yake mapya lakini jibu lake lilikuwa rahisi ‘Nimeamua kubadilika!’ Hatimaye wengine walitamani kuishi kama yeye. Karibu kusikiliza ushuhuda wa maisha ya kijana Ebenezer mfanyakazi wa Soma Biblia katika tawi la Arusha.

Ebenezer Shafuli 2 (2).jpg

Ushuhuda wa Melania Joakim 'Yesu alinichagua bila gharama yoyote'

Cathbert Msemo

Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni

Karibu kusikiliza ushuhuda wa Melania Joakim kuhusu jinsi alivyopata neema ya kumjua Mungu. Alijiunga tu nawenzake kwenda Shule ya Jumapili wakati akiwa mdogo. Pamoja na kwamba wazazi wake hawakuwa wakristo, hakukatazwa kuendelea kwenda Kanisani. Kupitia yeye sasa mama yake amashampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuna mengi ya kujifunza katika ushuhuda wake. Alifunuliwa habari za upendo mkuu wa Yesu aliposoma Yohana 15:16, Yaani Mungu ametuchagua bila gharama yoyote? Ni neema ya ajabu sana. Melania ni mfanyakazi wa Soma Biblia kwa miaka mitano sasa.

Melania Joachim 2 (2).jpg

Ushuhuda wa Letesi Chuma 'Kweli Mungu Yupo'

Cathbert Msemo

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Huu ndio mstari ninao upenda sana Yohana 3:16. Nilitoka katika mazingira ya watu ambao hawajamjua Mungu. Sikujua kwenda Kanisani wala sikumjua Mungu. Lakini sasa mimi ni mwinjilisti nafanya kazi Soma Biblia. Letesi Chuma anatushirikisha ushuhuda wake wa namna alivyopata neema ya kumjua Mungu na kutoka katika mazingira ya Upagani. Karibu kusikiliza

20200603_131759 (2).jpg

Emma Victoria Kikimba 'Bwana Ndiye Mchungaji Wangu'

Cathbert Msemo

Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.

Emma Kikimba amezungumza na Vivi Houmaa Jørgensen na kutushirikisha safari ya maisha yake ya Ukristo. Zaburi ya 23 ni maneno anayoyapenda sana katika Biblia. Alianza kumjua Mungu utotoni katika Shule ya Jumapili na aliendelea kujifunza zaidi na kumwamini Yesu mpaka sasa. Karibu kusikiliza

20200603_134207.jpg

Eliya Abdahla Mhando 'Namwamini Yesu Kristo'

Cathbert Msemo

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Eliya Abdahla Mhando ni mfanyakazi wa Soma Biblia kwa miaka 30 sasa. Alijiunga na Soma Biblia mwaka 1987. Hakuwa Mkristo, lakini alisukumwa kufanya kazi ya kuuza vitabu vya Soma Biblia. Alijiunga na Bible study katika ofisi za Soma Biblia na siku moja alipata zawadi ya Biblia. Alipokuwa anasoma alikutana na mstari huu: Yohana 14:6. Hadithi yake ya kubadilika, kuokoka na kumpenda Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake, itakuvuta na kuendeleza kiu yako ya kumjua Mungu.

Karibu usikilize

20200603_134318 Eliy.jpg

SUBIRA: Nimelelewa katika familia ya Kikristo

Cathbert Msemo

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

“Neno hili la Yeremia 29: 11 linanipa tumaini kujua kila ninachokifanya sipo peke yangu bali Mungu yupo nyuma yangu akinitia nguvu. Mungu anatuwazia mawazo ya amani wala si mabaya”. Karibu kusikiliza mahojiano haya kati ya Bi. Vivi na Subira Joachim Ammy upate kujua jinsi Subira alivyoweza kuwa Mkristo mzuri tangu utotoni hadi leo.

20200526_113830 Subira (2).jpg