Neno la Injili kwa Rika Zote!
Soma Biblia ni nani?
Soma Biblia Society ni shirika la wahisani linalolenga kusambaza Injili ya Yesu Kristo kwa rika zote. Shabaha nyingine ni kuwasaidia Wakristo kufikisha Injili kwa watu na kuwafundisha kupitia neno la Mungu – juu ya imani na maisha. Baadhi ya kazi zetu ni pamoja na:
Kusambaza Biblia, Vitabu na Vifaa vya Kanisa
Tuna maduka na magari yanayosambaza Biblia za watu wazima na watoto, vitabu vya Kikristo pamoja na vifaa vya madhabahuni nchini kote.
Agiza BibliaTunachapisha Vitabu vya Kikristo
Tunachapisha vitabu vya mafundisho ya Biblia, ukuaji wa kiroho na maisha ya Kikristo kwa watu wa rika mbalimbali.
Nunua VitabuSoma Biblia kwa Njia ya Mtandao
Jifunze popote ulipo kupitia kozi zetu za mtandaoni ukiongozwa na walimu wenye uzoefu na kujifunza kwa wakati wako.
Jiunge na KoziUinjilisti na Misheni
Tunafanya uinjilisti, programu za vijana na kuwafikia watu wengi zaidi kwa Injili ya Yesu Kristo kupitia huduma mbalimbali.
Jiunge NasiSoma Biblia App
Nunua, soma, sikiliza na jifunze Neno la Mungu kupitia App yetu yenye maktaba ya Kiswahili, Kiingereza na vitabu vya bure.
Pakua AppBidhaa maarufu dukani
Tuna bidhaa nyingi. Hizi ni baadhi ya bidhaa zinazopendwa sana na wasomaji na Wakristo wengi.
HABARI KUTOKA SOMA BIBLIA
Neno la Injili
Kiganjani Mwako
10K+
Watumiaji wa App
500+
Vitabu na bidhaa
24/7
Inapatikana kila wakati
Kwa nini uchague Soma Biblia?
Tunakupa huduma zinazokusaidia kulijua Neno la Mungu, kukua katika imani na maisha.
Ukuaji wa huduma yetu
Kwa miaka mingi, Soma Biblia imeendelea kuwa chombo cha kusaidia Kanisa na jamii kwa kusambaza Biblia, vitabu vya Kikristo na vifaa vya madhabahuni, vyote vikiwavuta watu kukua katika Neno la Mungu.
Tuna Aina Nyingi za Biblia
Biblia ni Neno la Mungu. Sisi tumeendelea kuwa chombo cha usambazaji kwa Kanisa na Jamii.
Vitabu na Vifaa vya Kanisa
Tunasambaza vitabu vya Kikristo ili watu wapate vifaa muhimu vya kujifunza Habari Njema za Wokovu wa Yesu Kristo.
Tupo Kidijitali
Tunawafikia watu wengi kupitia tovuti, mitandao ya kijamii na App ya Soma Biblia.
Maduka ya Soma Biblia
Tunahakikisha tunawafikia Wakristo karibu ili wapate Maandiko na vifaa muhimu kwa gharama nafuu.
Miaka ya Huduma
Soma Biblia imeendelea kuhudumu, kukua na tupo tayari kusonga mbele.
Maduka Yanayotembea
Magari yetu ya vitabu husafiri katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ili kuwafikishia watu Biblia na vitabu vya Kikristo.
Chagua Duka
Bofya duka lolote hapa chini au alama kwenye ramani ili kuona eneo na taarifa za duka husika.
Main Office — Barabara ya Mwai Kibaki, Mikocheni B, Dar es Salaam.
Taarifa za Duka Fungua kwenye Google MapsSoma Biblia katika video
Tazama video mbalimbali zinazokusaidia kufahamu zaidi kuhusu Soma Biblia, huduma zetu, bidhaa na kazi yetu katika kusaidia Kanisa na jamii kukua katika Neno la Mungu.
Tazama zaidi kutoka Soma Biblia
Duka la Soma Biblia
Angalia vitabu, Biblia na rasilimali za kujenga imani yako kila siku.
VIDEO
Dini na Maisha
Tafakari maswali muhimu kuhusu imani, maisha na uhusiano wetu.
VIDEO
Katikati ya Majambazi
Filamu yenye ujumbe kuhusu maisha, changamoto, uchaguzi na matumaini.
FILAMU
Ushuhuda wa wateja
Tunashukuru kwa watu wote wanaotumia vitabu na huduma za Soma Biblia.
Nimesoma vitabu vingi kutoka Soma Biblia, vimenisaidia sana kukua katika imani.
Soma Biblia ni msaada mzuri kwa Wakristo, tunapata Biblia na vitabu kwa urahisi.
Vitabu vya Soma Biblia vimenisaidia kupata maarifa na kujenga maisha yangu ya kiroho.
Ungependa kujua zaidi kuhusu Soma Biblia?
Tumekusanya majibu ya maswali muhimu kuhusu oda, malipo, usafirishaji, App, kozi za mtandaoni na huduma za uchapishaji.
Unaweza kuagiza Biblia na vitabu vya Kikristo kupitia huduma za Soma Biblia. Kwa oda, upatikanaji wa kitabu au usafirishaji, wasiliana na Sales Manager au Main Office.
Gharama ya usafirishaji hutegemea eneo lako, ukubwa wa oda na njia ya usafirishaji. Kwa kiasi sahihi, wasiliana na Sales Manager kabla ya kuthibitisha oda.
Ndiyo. Soma Biblia App ina huduma na maudhui ya bure, huku baadhi ya vitabu na maudhui yakipatikana kwa ununuzi.
Kwa msaada kuhusu App, unaweza kumtafuta Cathbert Msemo au Jeremiah Msuya.
Utapewa maelekezo sahihi ya malipo wakati wa kuthibitisha oda yako. Kwa masuala ya malipo, uthibitisho wa fedha au risiti, wasiliana na Finance Manager.
Soma Biblia ina maduka katika maeneo mbalimbali Tanzania na pia husambaza Biblia na vitabu kupitia huduma za usafirishaji na mobile bookshops. Kwa eneo lako, wasiliana na Sales Manager.
Ndiyo. Unaweza kuchagua kuchukua oda yako kwenye duka la Soma Biblia baada ya oda kuthibitishwa. Tunashauri uthibitishe kwanza upatikanaji wa kitabu.
Wasiliana na Sales Manager au Main Office ili kuthibitisha upatikanaji wa kitabu kabla ya kuagiza.
Unaweza kujiunga kupitia Soma Biblia App au tovuti ya Soma Biblia. Kozi hizi zimeandaliwa kwa ajili ya kujifunza mafundisho ya Kikristo kwa njia ya mtandao.
Kozi ni bure isipokuwa gharama ya kitabu kinachohitajika kwenye kozi. Pia kuna Mshauri wa Kozi wa kukusaidia wakati wa kujifunza.
Ikiwa wewe ni mwandishi na ungependa kitabu chako kichapishwe au kisambazwe na Soma Biblia, wasiliana na Idara ya Uchapishaji ili kufahamu utaratibu na mahitaji ya kuwasilisha kazi yako.
Kwa maswali ya jumla kuhusu Soma Biblia, huduma zetu au jambo ambalo hujui ni idara gani inayohusika, unaweza kuanza kwa Main Office.
Kwa suala linalohitaji uongozi wa juu, unaweza kumtafuta Soma Biblia Director.
Kwa masuala ya malipo, uthibitisho wa fedha, risiti au taarifa za kifedha, tafadhali wasiliana moja kwa moja na Finance Manager.
Hatujapata swali hilo
Jaribu kutumia maneno mengine kutafuta swali lako.
Wasiliana nasi.
Hujapata jibu unalotafuta? Wasiliana moja kwa moja na timu ya Soma Biblia.
Tuanze pamoja Kusoma Vitabu na Biblia
Pata Biblia, vitabu vya Kikristo, mafundisho na vifaa mbalimbali vitakavyokusaidia kukua katika imani, kulijua Neno la Mungu zaidi na kupokea wokovu kupitia Yesu Kristo.
Nikukaribishe kusoma toleo hili. Linatufundisha kusema hapana kwa yale yasiyo mapenzi ya Mungu. Makala zote zitatutia moyo na kutujengea ujasiri wa kusema hapana. Mfano mzuri ni Danieli na rafiki zake walivyomwambia Mfalme (tazama uk.15). Kwa vijana kuna makala muhimu sana juu ya kutunza miili yetu. Na usisahau michezo na katuni kuhusu Dada Rehema na wadogo zake. TSH. 500 TU.