Katika maisha haya watu wengi wanatumia damu ya Yesu kwa mambo mengi. Lakini je, matumizi haya yote ni sawa? Soma toleo hili lenye kichwa ‘Neema Yatosha’. Ndani yake kuna makala ya “Kwa damu ya Yesu” inatafakari swali hili zaidi. Pia utasoma mada kuhusu damu ya Yesu ilivyo na maana kwa ushirika wetu kama Wakristo pamoja na ushuhuda wa kukutia moyo wakati unapoona ni kana kwamba Mungu hasikii maombi yako ya muda mrefu.
Soma Riziki hapa Bure
Read More
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna tunavyoweza kufikia maisha kwa kuandaa viongozi walio bora kuanzia katika umri wa ujana. Nia ni kuliamsha kanisa kama taasisi muhimu na ya kuaminika katika kuandaa viongozi wenye hofu ya Mungu, wenye maadili mema, wachapa kazi na walio tayari kuacha maslahi yao kwa ajili ya wengine.
Read More
Mradi mpya wa kupeleka habari njema ya Yesu Kristo kwa vijana wanaokaa Arusha umeanza. Soma Biblia tumetembelea Shule ya Sekondari Sombetini na kuwagawia wanafunzi karibu na 1500 nakala ya kijitabu cha Masiha. Wote walipenda kupata zawadi hii.
Read More
Soma Biblia tuna mradi mpya wa kufikisha Injili kwa vijana kupitia kijitabu kinachoitwa Masiha. Kwa njia ya vibonzo, kijitabu hicho kinasimulia habari za Agano Jipya kuhusu maisha ya Yesu hapa duniani tangu kuzaliwa kwake mpaka alipopaa Mbinguni. Ni pamoja na mafundisho yake, na kusulubiwa, kufa na kufufuka kwake.
Read More