RIZIKI TOLEO LA #2/2023 - 'Linapatikana'
Cathbert Msemo
"Vijana wanaandaliwaje kabla ya ndoa?"
Siku moja niliwauliza vijana mahali fulani swali hili, Je, ni jambo gani utalipa kipaumbele kama la kwanza ukifikia umri wa kuoa au kuolewa? Jibu nililopata lilinishangaza kidogo. Kijana huyu alisema, “Mimi bro nitaangalia uzuri wa sura tu, tabia tutarekebishana huko ndani ya ndoa”.
Jibu hili na mengine mengi ambayo umewahi kuyasikia, yananipa swali la kujiuliza, Hivi nani anawaandaa vijana wetu kuwa wanandoa wazuri siku za mbeleni? Je, semina za wiki kadhaa kabla ya kufunga ndoa zinatosha kutoa mafundisho ya kuwaandaa vijana kuelekea kwenye ndoa?
Katika toleo la pili la gazeti la Riziki tunajadiliana kichwa kisemacho, Vijana wanaandaliwaje kabla ya ndoa? Lengo la mada hii ni kuchochea na kuamsha mjadala juu ya kuandaa vijana wanaotarajiwa kuingia katika ndoa katika misingi ile aliyoiweka Mungu ili hata ndoa zao zitakapopata mitikisiko, bado waweze kusimama katika kumtegemea Mungu.
Katika gazeti hili utakutana na kisa kimoja cha binti aliyeandaliwa vizuri kuwa mke mwema. Zaidi sana alifundishwa ukarimu, heshima na bidii ya kufanya kazi. Hata alipokutana na mgeni kisimani, alikuwa tayari kumhu-dumia yeye pamoja na ngamia wake bila kujua kuwa alikuwa mgeni maalumu kwenye nyumba ya baba yake.
Pamoja na hayo utakutana na makala zenye shuhuda, wimbo na mafundisho ya kukujenga na kukuimarisha katika safari yako ya ndoa.
UNAWEZA KUSOMA RIZIKI ONLINE BURE. BONYEZA LINK HAPA