RIZIKI TOLEO 03/2023 - Linapatikana
Cathbert Msemo
Tufundishe Watoto Wetu
Kila mwaka makanisa mengi huwa na sikukuu za watoto. Hii ni siku maalumu, na watoto wengi huingojea kwa hamu. Ni siku ambayo vyakula na vinywaji maalumu huandaliwa kwa ajili yao. Tena kunakuwa na shamrashamra nyingi kwa watoto. Hata watoto ambao huwa hawaji kanisani, siku hii wapo. Ni siku kuu kwa watoto.
Lakini je, mahubiri ya siku hii yanawalenga akina nani hasa? Ni kwa ajili ya wazazi wanaowalea watoto au ni kwa ajili ya watoto ambao kimsingi ndio wenye siku yao?
Mada kuu ya toleo la tatu la Riziki inasema “tuwafundishe watoto wetu“. Lengo la mada hii ni kukumbushana kama familia, kanisa na jamii kuweka mkazo katika malezi ya watoto. Ni changamoto kubwa, hasa katika nyakati za leo ambako kuna uharibifu na ukatili wa kila namna kwa watoto.
Katika gazeti hili utakutana na kisa cha baba mmoja ambaye licha ya kuwa utumwani, alikuwa na jukumu la kumlea binti yatima ambaye baadaye alikuja kuwa mkombozi wa watu wake ambao adui alilenga kuwaua kwa hila. Licha ya kuwa mwanaume, tena utumwani, bado alimwongoza binti huyu katika malezi mema na katika njia ya Bwana.
Pia utapata somo la mahubiri la sikukuu ya watoto 2023 na ushuhuda wa kijana, ambaye alipata changamoto ya malezi, lakini Mungu alinusuru maisha yake. “Na watoto wako wote watafundishwa na BWANA; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi” ( Isa 54:13).
Karibu kusoma RIZIKI ONLINE BURE. BOFYA HAPA