TWENDE TOLEO LA 3/2022 Linapatikana
Cathbert Msemo
‘Nimesamehewa’
Katika toleo hili tutajifunza juu ya msamaha.
Inatokea tunafanya makosa, sivyo? Tukiwakosea marafiki, ndugu au wazazi wetu, huharibu uhusiano wetu nao. Zaidi sana makosa yanaharibu uhusiano wetu na Mungu. Makosa hayo ni kinyume na mapenzi yake na huitwa dhambi.
Je, tunarudishaje uhusiano ulioharibika? Haisaidii kujificha tusionane na yule tuliyemkosea. Hata kama akitaka tu kutusamehe, ni lazima tumwone tukikiri kosa na kuomba msamaha.
Vivyo hivyo na uhusiano wetu na Mungu. Katika makala ya Sala Mfalme Daudi anaeleza alivyojisikia ali-pomficha Mungu dhambi, na matokeo yake alipomjulisha Mungu alivyomkosea.
Mungu yupo tayari kutusamehe tukifanya kama Daudi. Ni kwa sababu Yesu alichukua hukumu yetu ya adhabu juu yake alipokufa. Kwa hiyo Mungu hamhe-sabii dhambi mtu yule anayekuja kwa Yesu kuomba msamaha.
Kusamehewa na Mungu hufungamana na sisi kuwasamehe wanaotukosea. Katika makala ya Sala ya vijana Yusufu anatoa mfano mzuri wa kutoa msamaha.
Kama kawaida kuna kibonzo kizuri. Angalia katika uk.5 unavyoweza kupata zawadi kama ukijibu maswali vizuri! Pia Kaka Kalamu anakukumbusha atakujibu kama ukimwandikia swali lako. Karibu tusome!
TWENDE LINAUZWA TSH. 500 TU. Karibu dukani Soma Biblia