RIZIKI TOLEO LA 3/2022 linapatikana
Cathbert Msemo
‘Tumeitwa kutenda mema’
Toleo hili la Riziki linaongozwa na mada isemayo “Tumeitwa kutenda mema”. Msingi wa mada hii unatokana na ukweli kwamba tunaishi katika nyakati ambazo ukatili na kutokuthaminiana kumekuwa kwa kiwango cha juu sana. Lakini pia majadiliano yanaenda zaidi, maana kutenda mema peke yake hakutoshi kama una tarajio la kuurithi uzima wa milele.
Katika toleo hili utakutana na kijana wa miaka 33 ambaye katika umri wake huo alitenda mema mengi kwa kila aliyemjia na kumhakikishia uzima wa milele. Unataka kumjua mtu huyo wa ajabu ni nani? Fungua gazeti lako usome habari za mtu huyo.
Pia ndani ya gazeti utakutana na makala mbalimbali zenye maonyo na kufundisha juu ya ukatili, shuhuda na wimbo wa kukutia moyo wewe ambaye unatamani kuunganisha matendo mema na toba ya kweli.
Bonyeza hapa kusoma RIZIKI ONLINE BURE