Katika toleo hili tutajifunza jambo la muhimu sana tunapotaka kumpendeza Mungu na wanadamu. Jambo hili ni UTII. Kutii ni pamoja na swali gumu. Je, nimtii Mungu au mwanadamu? Wewe umewahi kujiuliza hivyo? Karibu kusoma toleo hili. TSH. 500 tu.
Read More
Karibu kusoma toleo hili ujifunze zaidi juu ya Yesu rafiki yetu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hili. Tsh. 500 tu.
Read More
Soma Biblia tunapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Tuko tayari kuchangia ili furaha na baraka ya sikukuu ya watoto iendelee muda mrefu. Inawezekana ikiwa watoto wanapewa zawadi ya kudumu zaidi ya chakula kizuri. Kwa hiyo tunatoa ofa maalumu ya vitabu fulani vinavyowafaa watoto pamoja na walezi wao wote wanaowafundisha imani na maisha ya Kikristo. Tazama picha kuona vitabu na bei ya punguzo
Read More
Katika toleo hili utaweza kuelewa zaidi upendo wa Yesu kwetu sisi wanadamu. Kupitia makala ya Simulizi kwa mfano utasimuliwa jinsi Yesu alivyokasirika kuona wanafunzi wake wakiwakataza watoto wasiende kwake. Unajua Yesu alifanya nini siku hiyo? Karibu usome! Na usisahau makala nyingine, vibonzo na michezo. Yote yatakupa uelewa zaidi juu ya upendo wa Mungu kwetu.
Bonyeza hapa kupata orodha ya bei ya vitabu mbali mbali na Biblia
Read More
Katika toleo hili tunajifunza juu ya 'Kukaza Mwendo'. Kupitia makala mbalimbali tutajifunza maana hasa ya kukaza mwendo kwenda Mbinguni, na zaidi tuta-elewa kuwa sisi ni washindi tunaoweza kuzishinda changamoto za dunia hii kwa sababu yupo mmoja ambaye anatuwezesha kushinda tukiwa naye.
Kuna kibonzo kitakachokufurahisha na kukufundisha kukaza mwendo bila kukata tamaa hadi kufikia ushindi. Usisahau dada Rehema! Ana michezo na ukijibu maswali vizuri unapata zawadi. Pia Kaka Kalamu anakukumbusha kumwandikia kama una swali, naye atakujibu. Karibu tusome!
Read More
Katika toleo hili la Twende tutajifunza zaidi kuhusu agano letu na Mungu. Ndiyo, hata sisi tunaweza kufanya agano na Mungu. Ubatizo wa Kikristo ni agano la aina hii. Vilevile utasoma kuhusu watoto waliomwahidi Mungu jambo fulani. Kama una swali kuhusu agano, karibu kumwandikia Kaka Kalamu. Yuko tayari kujibu, mia kwa mia! Karibu kununua katika maduka ya Soma Biblia kwa Tsh. 500/= tu.
Read More
Katika toleo hili tumefafanua mengi juu ya imani kukua. Kwa mfano, Joni na Jeni wanasikia habari kuhusu imani, na wanavutwa kumuuliza Rehema swali; Imani ni nini?. Mazungumzo yao na majibu ya Rehema ni katika katuni. Pia kuna michezo ya kuvutia. Usisahau kututumia majibu yako kama ilivyoelekezwa kwenye uk.5 na nyuma ya gazeti.
Read More
Karibu kununua TWENDE kwa Tsh. 500 tu katika maduka ya Soma Biblia. Toleo hili linafafanua juu ya Uhusiano wetu na Mungu. Kwa njia ya simulizi na hadithi nzuri utaweza kuelewa juu ya jambo hili. Utakutana pia na Dada Rehema na wenzake, na kuna michezo ya kuvutia. Usisahau kututumia majibu yako kama ilivyoelekezwa kwenye uk.5 na nyuma ya gazeti.
Read More
Habari hii njema tunafafanua zaidi katika toleo hili. Na wewe Kijana mpendwa, usisahau kuna makala nzuri kwa ajili yako pia. Inahusu miiba. Lakini Yesu yupo kukulinda isikuchome!
Read More
Umewahi kusikia mtu akisema, “Mimi ni mwanafunzi wa Yesu”? Au, “Mimi ni mtoto wa Yesu? Au, “Mimi ni mtumishi wa Yesu? Je, ana maana gani hasa? Soma makala za gazeti hili upate ufafanuzi mzuri kuhusu swali hili.
Read More
Mpendwa msomaji wa Twende, uvumilivu ni tunda la Roho tunayepewa tunapomwamini Yesu. Biblia inatufundisha uvumilivu kupitia watu mbalimbali. Toleo hili limefafanua zaidi maana ya uvumilivu kwetu sisi Wakristo. Jipatie nakala yako kutoka Soma Biblia.
Read More
Miezi iliyopita tumekuwa busy sana hapa Soma Biblia. Tumechapa matoleo jipya ya Twende na RIZIKI, tumefanya semina ya wafanyakazi wote, na kitabu kipya kimetolewa. Karibu kusoma zaidi!
Read More