Twende toleo la 4/2024 'linapatikana'
Cathbert Msemo
Sisi ni Kanisa la Mungu
MPENDWA MSOMAJI
Bila shaka umewahi kuona jengo kubwa nzuri na kujua kuwa hilo ni kanisa. Mara nyingi majengo hayo yana mwonekano tofauti na majengo mengine. Kwa mfano mengi yana mnara wenye msalaba juu yake. Hivyo ni rahisi kutambua kuwa hili ni kanisa.
Pia majengo hayo yana majina yanayotuambia ni kanisa. Kwa mfano utaona kumeandikwa KKKT, kisha jina la dayosisi na usharika. Au Kanisa Katoliki jimbo la ... kisha jina la Parokia.
Ni sawa kabisa kuyaita majengo haya kanisa. Maana yake ni mahali pa kuabudia ambapo pia kunaratibiwa shughuli mbalimbali zinazohusu wanaosali hapo. Lakini je, unajua kuna maana nyingine ya kanisa, tena iliyo kubwa na ya muhimu sana kwetu Wakristo kuielewa?
Katika toleo hili tutaagalia maana ya Kanisa, herufi K ikiwa kubwa. Kanisa hili si jengo bali ni sisi tunaomwamini Yesu Kristo. Ndiyo maana tunasema, "Sisi ni Kanisa la Mungu".
Katika makala ya hadithi, kwa mfano, utaona mtoto ambaye alipata kuelewa jambo hili akiwa katika Shule ya Jumapili. Na wewe utaweza kuelewa kupitia makala za toleo hili. Nikukaribishe sana kusoma! Na kule mwishoni usisahau kuchunguza pamoja nami Biblia yako ili kujifunza zaidi maana ya Kanisa.
Karibu kusoma toleo hili kwa Tsh. 500 tu.