Katika toleo hili tutajifunza juu ya msamaha.
TWENDE ni gazeti la Kikristo kwa Watoto na Vijana. Kupitia gazeti hili, tunataka kufundisha Watoto na vijana Injili ya uzima wa milele ndani ya Yesu Kristo. TWENDE inatolewa mara nne kwa mwaka. Bei: 500 Tsh kwa nakala moja. Karibu dukani Soma Biblia
Read More
Toleo hili la Riziki linaongozwa na mada isemayo “Tumeitwa kutenda mema”. Msingi wa mada hii unatokana na ukweli kwamba tunaishi katika nyakati ambazo ukatili na kutokuthaminiana kumekuwa kwa kiwango cha juu sana. Lakini pia majadiliano yanaenda zaidi, maana kutenda mema peke yake hakutoshi kama una tarajio la kuurithi uzima wa milele.
Bonyeza HAPA kusoma bure
Read More
Katika toleo hili la Riziki tunajadili mada isemayo, Je, Mungu anaweza kumwacha mwanadamu? Msingi wa swali hili unatokana na hali ambazo tunakutana nazo kwenye maisha. Kuna wakati unapita mahali pagumu na kufikia hatua ya kufikiri kwamba Mungu amekuacha. Bila shaka, wakati wa shida na uhitaji mkuu ungetamani kuona mtu unayehusiana naye vyema akiwa karibu nawe kukutia moyo na kukusaidia. Vipi usipomwona, unajisikiaje?
Karibu kusoma zaidi Hapa bure
Read More
Katika toleo hili tunajifunza juu ya 'Kukaza Mwendo'. Kupitia makala mbalimbali tutajifunza maana hasa ya kukaza mwendo kwenda Mbinguni, na zaidi tuta-elewa kuwa sisi ni washindi tunaoweza kuzishinda changamoto za dunia hii kwa sababu yupo mmoja ambaye anatuwezesha kushinda tukiwa naye.
Kuna kibonzo kitakachokufurahisha na kukufundisha kukaza mwendo bila kukata tamaa hadi kufikia ushindi. Usisahau dada Rehema! Ana michezo na ukijibu maswali vizuri unapata zawadi. Pia Kaka Kalamu anakukumbusha kumwandikia kama una swali, naye atakujibu. Karibu tusome!
Read More
Nina mashaka, nifanye nini?
Tunapoelekea sehemu ya mbali na ni mara ya kwanza kupita katika njia ile, tunakuwa makini tusipotee. Hali ya safari inakuwa na changamoto zaidi pale tunapokutana na njia zaidi ya moja. Je, tufuate njia ipi?
Ndani yetu kunaweza kujengeka mashaka kuwa tupo karibu na kupotea. Lakini tunapopata kuelewa na kuifuata njia iliyo sahihi, tunapata tena furaha ya safari.
Mtoto mwenzangu, jambo hili hutokea pia katika safari yetu ya imani. Wakati mwingine changamoto ikitukuta njiani, tumaini letu linapotea, na tunapata woga na wasiwasi mkubwa. Je, tufanye nini?
Yesu anatuambia, 'Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha' (Mathayo 11:28). Yesu anaweza kutuondolea mashaka yote tuliyonayo. Unajua anafanyaje?
Toleo hili linafafanua jinsi kuu ya kuondokana na mashaka, nayo ni kumfuata Yesu. Yeye ni Mungu pamoja nasi. Kupitia makala mbalimbali, michezo na katuni, utajifunza na kuelewa zaidi habari hii njema.
Karibu kununua dukani Soma Biblia kwa 500/= tu.
Katika toleo hili la kwanza la Riziki kwa mwaka huu 2022, tunajadili masuala ya kipindi cha Kwaresima. Kanisa na waumini wake hufanya nini, na kwa nini? Na je, njia ipi ni bora zaidi, ukitaka kutumia vema kipindi hiki cha siku 40 kabla ya Pasaka?
Utakutana na kijana mmoja ambaye alitoa wito wa ajabu kwa wanafunzi wenzake akiwaambia, “Twendeni nasi tukafe naye” (yaani, Yesu).
Utapata pia makala mbalimbali za kukujenga na kukuimarisha kiroho, na kukusogeza karibu na Mungu. Katika majira haya ya Kwaresima naungana na nabii Yoeli kwa maneno haya, “Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya” (Yoe 3:13).
SOMA BURE HAPA, RIZIKI
Katika toleo hili la Riziki tunajadili kuhusu nguvu ya msalaba. Ni mahali ambapo Yesu Kristo alitundikwa yapata miaka elfu mbili iliyopita, lakini tukio lile lilisababisha mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu. Ni tukio hili ambalo lilirudisha uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Yeye ambaye hapo kwanza alikuwa amegombana na Baba yake wa mbinguni, sasa amerudishiwa nafasi yake kama mtoto na mrithi pamoja na Kristo.
Read More
Soma Biblia kila siku 2022
ni vitu vitatu kwa wakati mmoja
Kalenda ya mfukoni
Mpango wa usomaji wa Biblia mwaka mzima
Ufafanuzi wa somo la Biblia
Read More
Katika toleo hili la Twende tutajifunza zaidi kuhusu agano letu na Mungu. Ndiyo, hata sisi tunaweza kufanya agano na Mungu. Ubatizo wa Kikristo ni agano la aina hii. Vilevile utasoma kuhusu watoto waliomwahidi Mungu jambo fulani. Kama una swali kuhusu agano, karibu kumwandikia Kaka Kalamu. Yuko tayari kujibu, mia kwa mia! Karibu kununua katika maduka ya Soma Biblia kwa Tsh. 500/= tu.
Read More
Sisi wa Soma Biblia tunapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Tuko tayari kuchangia ili furaha na baraka ya sikukuu ya watoto iendelee muda mrefu. Inawezekana ikiwa watoto wanapewa zawadi ya kudumu zaidi ya chakula kizuri. Kwa hiyo tunatoa ofa maalumu ya vitabu fulani vinavyowafaa watoto pamoja na walezi wao wote wanaowafundisha imani na maisha ya Kikristo.
Read More
Sasa Biblia mpya ya lugha mbili inapatikana dukani Arusha, na Ebenezer anawakaribisha kwa furaha kubwa wateja wote. Pia katika matawi mengine ya Soma Biblia, yaani Mwanza, Iringa, Mbeya na Dar es Salaam Biblia hii inapatikana. Karibu upate nakala
Read More
Katika toleo hili tumefafanua mengi juu ya imani kukua. Kwa mfano, Joni na Jeni wanasikia habari kuhusu imani, na wanavutwa kumuuliza Rehema swali; Imani ni nini?. Mazungumzo yao na majibu ya Rehema ni katika katuni. Pia kuna michezo ya kuvutia. Usisahau kututumia majibu yako kama ilivyoelekezwa kwenye uk.5 na nyuma ya gazeti.
Read More
Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya nne, Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Mikononi mwa Mu-ngu majaribu yanaweza kuimarisha imani yetu na kutupa uzoefu kwamba Mungu ni mwaminifu na mwenye uwezo wa kutupitisha salama kiroho. Tunapopatwa na majaribu, kisha tukavuka salama, imani yetu huwa inaongezeka. Yesu anatuombea kila wakati; tulindwe na yule mwovu. Lengo la ombi hili ni kwamba, hata katikati ya majaribu, tulindwe dhidi ya hila za yule mwovu na tuvuke salama.
Ndani ya toleo hili utakutana na watu waliopita katika majaribu yaliyogusa kila eneo la maisha yao. Hata hivyo walisimama katika imani, na hatimaye walitoka wakiwa kama dhahabu safi ing’aayo. Siri yao ikoje? Soma makala za toleo hili, na ujifunze – kwa ajili ya maisha yako mwenyewe ili uweze kuwasaidia vema wanaojaribiwa!
Read More
Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya tatu, Utusamehe makosa yetu, kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea. Msamaha ni jambo lenye nguvu sana. Tunapenda sana msamaha, lakini mara nyingi tunapotakiwa kukiri makosa yetu au kuwasamehe waliotukosea, tunaliona kuwa jambo gumu. Tunapenda kupokea msamaha lakini hatupendi kuutoa.
Read More
Soma Biblia tuna mfululizo wa vitabu hivi: Tafakuri za Neno la Mungu 'Siku kwa Siku na Mungu'. Kila siku unapata nafasi ya kumtafakari Mungu kupitia somo la siku husika katika vitabu hivi kwa mwaka mzima. Vitabu hivi vimetolewa kama zawadi, hivyo ni bei rahisi kupata nakala. Kwa kila kitabu ni Tsh. 2000 tu.
Read More
Toleo hili la RIZIKI ni muendelezo wa kuangalia Sala ya Bwana, sehemu ya pili isemayo “Utupe leo riziki yetu”. Sehemu hii inatufundisha kumwendea Mungu kwa moyo wa unyenyekevu na kumtegemea, tukimwomba atupe riziki yetu ya kila siku. Tunatiwa moyo tupeleke mahitaji yetu yafahamike kwa Mungu, tukiamini kuwa tutapewa. Kwa kuomba hivi tunakubali kwamba, kila tunachohitaji kwa ajili ya maisha yetu ya leo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Read More
Karibu kununua TWENDE kwa Tsh. 500 tu katika maduka ya Soma Biblia. Toleo hili linafafanua juu ya Uhusiano wetu na Mungu. Kwa njia ya simulizi na hadithi nzuri utaweza kuelewa juu ya jambo hili. Utakutana pia na Dada Rehema na wenzake, na kuna michezo ya kuvutia. Usisahau kututumia majibu yako kama ilivyoelekezwa kwenye uk.5 na nyuma ya gazeti.
Read More
Mwaka mpya 2021 unakaribia. Umeshanunua kalenda ya ukutani? Soma Biblia tumekuandalia kalenda nzuri. Karibu kununua katika maduka yetu ya Soma Biblia
Read More
Karibu kusoma mpango wa Soma Biblia Kila Siku kwenye YouVersion bure.
Read More
Biblia ni taa ya miguu yake aishiye na Mungu. Soma Biblia tuna zana nzuri za kusoma Neno la Mungu kila siku. Soma Biblia kila siku 2021 ni Kalenda kamili na ufafanuzi kila siku kwa somo la Biblia
Karibu kununua nakala yako mapema katika maduka yetu ya Soma Biblia ili usichelewe kuanza mpango wa kusoma Biblia mwaka 2021.
Read More