TWENDE TOLEO LA #1,2022
Cathbert Msemo
Nina mashaka, nifanye nini?
Tunapoelekea sehemu ya mbali na ni mara ya kwanza kupita katika njia ile, tunakuwa makini tusipotee. Hali ya safari inakuwa na changamoto zaidi pale tunapokutana na njia zaidi ya moja. Je, tufuate njia ipi?
Ndani yetu kunaweza kujengeka mashaka kuwa tupo karibu na kupotea. Lakini tunapopata kuelewa na kuifuata njia iliyo sahihi, tunapata tena furaha ya safari.
Mtoto mwenzangu, jambo hili hutokea pia katika safari yetu ya imani. Wakati mwingine changamoto ikitukuta njiani, tumaini letu linapotea, na tunapata woga na wasiwasi mkubwa. Je, tufanye nini?
Yesu anatuambia, 'Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha' (Mathayo 11:28). Yesu anaweza kutuondolea mashaka yote tuliyonayo. Unajua anafanyaje?
Toleo hili linafafanua jinsi kuu ya kuondokana na mashaka, nayo ni kumfuata Yesu. Yeye ni Mungu pamoja nasi. Kupitia makala mbalimbali, michezo na katuni, utajifunza na kuelewa zaidi habari hii njema.
Karibu kununua dukani Soma Biblia kwa 500/= tu.