TWENDE TOLEO LA #03/2021 'Linapatikana'
Cathbert Msemo
Agano langu na Mungu
Jambo kuu la toleo hili la Twende ni Agano. Tunapoahidiana jambo, tunaweza kusema ni agano. Kwa kufanya agano tunajiwekea sharti la kuitimiza ahadi yetu. Lakini mara nyingine tunaivunja ahadi yetu kwa kukusudia, au tunashindwa kwa sababu hatukujua huko mbele hali yetu itakuwaje.
Sasa kuna mmoja ambaye daima anatimiza ahadi zake za agano. Ni Mungu. Ahadi zake ni za kweli. Tukisoma Biblia tunaona mifano mingi ya watu waliopewa agano na Mungu, na ahadi zake zikatimia.
Katika toleo hili la Twende tutajifunza zaidi kuhusu agano letu na Mungu. Ndiyo, hata sisi tunaweza kufanya agano na Mungu. Ubatizo wa Kikristo ni agano la aina hii. Vilevile utasoma kuhusu watoto waliomwahidi Mungu jambo fulani.
Kama una swali kuhusu agano, karibu kumwandikia Kaka Kalamu. Yuko tayari kujibu, mia kwa mia!
Karibu kununua katika maduka ya Soma Biblia kwa Tsh. 500 tu.