RIZIKI TOLEO LA 1, 2019 - 'Ukristo ni utamaduni au imani?'
Cathbert Msemo
“Siendi kwa mazoea”
Katika toleo hili la RIZIKI tunachunguza kama Ukristo ni imani au utamaduni. Nia ni kukumbushana kuwa, mapokeo ya dini yanaweza kuwa mazoea au taratibu tupu zisizo na faida. Kama mwandishi mmoja alivyoandika, ndivyo taratibu zilivyo kama misingi yake haikujengwa katika Kristo. Lakini vilevile tamaduni na mapokeo zitafaa, tena zitakuwa na faida, kama zinatuelekeza kumwamini Yesu na kufanya mapenzi yake.
Ndani ya toleo hili utakutana na kijana ambaye baba yake alishika taratibu na tamaduni za Kiyunani, lakini bibi yake na mama yake walimwongoza katika kumwamini Yesu. Soma kuhusu chaguo lake kijana huyu, na yakatokea nini baadaye katika maisha yake.
Pamoja na makala nyingine nyingi, ni maombi yangu ukaimarike katika imani na kumjua Mungu zaidi na zaidi.