TWENDE toleo la 3, 2019 linapatikana
Cathbert Msemo
Umewahi kujisikia huna thamani? Huenda ulishindwa kuvaa nguo ya kupendeza kama wengine kwenye sikukuu, na marafiki zako wakakucheka. Inaumiza, sivyo?
Nikuambie habari njema! Mungu ni tofauti sana na wanadamu. Kwake yeye sisi sote ni wa thamani!
Hebu fikiri kidogo kwamba sote tumetenda dhambi. Hivyo hatukustahili kitu kwa Mungu. Lakini alifanyaje? Alimtuma Yesu atukomboe na kutufanya watoto wake.
Kama Neno lake anasema, “Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu” (Isa 43:1). Huu ni upendo wa ajabu sana, sivyo? Bila kujali hali zetu wala umri wetu, Mungu ametufanya wa thamani.
Habari hii njema tunafafanua zaidi katika toleo hili. Na wewe Kijana mpendwa, usisahau kuna makala nzuri kwa ajili yako pia. Inahusu miiba. Lakini Yesu yupo kukulinda isikuchome!
Twende ni kwa ajili ya Watoto na Vijana na linauzwa kwa bei poa ya Shilingi mia tano tu. Karibu dukani kwetu ujipatie nakala yako.
Bonyeza mkoa uliopo kupata mawasiliano: Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Iringa, Mwanza