Taarifa mpya kutoka kwa Soma Biblia
Anne Gihlemoen
Je, unajua kwamba mwaka jana wasambazaji wa Soma Biblia waliuza Biblia na vitabu millioni 2,2?! Na katika nchini ya Tanzania, Soma Biblia ni msambazaji mkubwa wa tatu katika Biblia. Maana, pamoja tunajenga nchi ya Tanzania, lakini muhimu zaidi, tunajenga nchi ya Mungu.
Sisi kama shirika la Soma Biblia, tupo kila mahali. Tuna matawi tano, na kutoka kwa yale tano, tunatumia gari ya kutembea nchi mzima. Wengi wanatuuliza: Fedha inazozidi katika mauzo yetu zinaenda wapi? Je, tunazikula? Je, zinaingia kwa poketi ya wakurugenzi? Hapana! Hela zinazozidi tunazi invest kwa kwenda mahali ambao tunajua ni kiyu ya kumfahamu Mungu, na mahali ambao ni mbali au mahali ambapo hatuuzi sana. Hela zingine tunazi invest katika uchapisaji wa vitabu vipya, au magazeti yetu, ya RIZIKI (gazeti kwa ajili ya watumishi wa kanisa) na Twende (gazeti la watoto).
SEMINA YA WAFANYAKAZI
Ili kupata umoja katika shirika letu, na kutia moyo na kuongezea ufahamu wetu wafanyakazi wote, tunakutana katika semina mara moja kila mwaka. Mwaka huu tulikutana katika Amabilis Centre, Morogoro. Tulikuwa na muda mzuri. Elizabeth Lulu kutoka kwa Mzumbe University alitufundishia neno la Mungu. Na moja kutoka kwa chama cha Biblia alitufundisha kuhusu utafsiri ya Biblia. Jioni tulikuwa na michezo na muda ya kuongea vizuri, na kujenga urafiki.