Twende toleo 1/2024 'linapatikana'
Cathbert Msemo
Yesu Mfalme wa Wafalme
MPENDWA MSOMAJI
Mfalme ni kiongozi wa ufalme. Mfalme ana nguvu za kuamua kila kitu ndani ya ufalme wake. Ndiye anayefanya sheria, anapanga matumizi ya fedha. Anaweza kuamua nani aishi na nani afe.
Mfalme anaweza kuwa mzuri au mbaya. Akiwa mfalme mzuri anaonyesha upendo kwa watu wake, na hukumu zake ni za haki. Mfalme mbaya anafikiri juu ya maendeleo yake tu, na hana rehema kwa watu wake.
Katika historia ya dunia, tunaona kwamba ilikuwa ni kawaida wafalme walitaka ufalme mkubwa zaidi. Kwa hiyo walijaribu kupora nchi nyingine kila wakati! Hii ilimaanisha kwenda vitani na majeshi makubwa na silaha kali mara kwa mara. Wafalme hawa walidhamiria kuchukua ardhi kwa nguvu, hata kama itakuwa kwa njia ya kuwaua watu wengi wasio na hatia.
Yesu ni Mfalme wa wafalme! Yeye pia anataka kuongeza ufalme wake. Lakini njia yake ni tofauti kabisa na hizo za wafalme wa duniani. Yesu hatumii ukatili au vita kueneza ufalme wake. Anatumia upe-ndo, rehema na msamaha.
Karibu kusoma toleo hili ujifunze zaidi juu ya Yesu, Mfalme wa wafalme. Tsh. 500 tu.