FAMILIA YA KIKRISTO/The Christian Family
Anne Gihlemoen
Kitabu hiki cha kiada kinawaandaa vizuri wanandoa watarajiwa kwa kuelewa na kufanyia kazi mafundisho ya ndoa wanayopewa kanisani kabla ya kufunga ndoa. Mambo yameratibiwa kwenye vipindi sita, vyote vikiwa na mazoezi kabla na baada ya mafundisho ya kichungaji kutolewa. Kitabu hiki ni msaidizi kweli kwa kila anayefundisha na kushauri kuhusu ndoa.
Masomo 31 ya kitabu hiki ni chakula bora na cha kiroho kwa moyo wako. Utazidi kumpenda Yesu. Kitumike kwenye sala ya binafsi au ya kifamilia.
Makala 12 nyingine kuhusu maisha ya familia kwa mpango wa Mungu. Matatizo mbalimbali ya vijana yanajadiliwa. Mashauri mazuri yapo.
Makala 10 zenye mafunzo na maelekezo ya Biblia kuhusu maisha ya familia kwa mpango wa Mungu, k.mf. uzazi, fedha – na ndoa ya furaha!
Wote wamejaribu kuomba. Lakini mafumbo yapo, na kuomba vibaya pia. Kitabu hiki maarufu kimewasaidia wengi kujua baraka za maombi.
Kwa nini ugomvi hutokea katika ndoa? Mwandishi anabainisha sababu na kutoa mashauri mazuri yenye uwezo wa kuifanya ndoa kuwa imara.
Je, unafahamu maana yake na kuiona katika maisha yako, kwamba Yesu ndiye amani yako? Masomo 25 yanayokusaidia kuiona.