Wanawake wa Imani - Vipindi sita kuvisikiliza
Anne Gihlemoen
Je, umezingatia kwamba sisi wanawake tunacho kitu kama sanduku mioyoni mwetu. Sehemu inayopaswa kujaa upendo. Ni jinsi Mungu alivyotuumba. Lakini mara nyingi ninasikia utupu hapo, au tuseme nina kiu. Kiu ya kupendwa. Ebu fikiria ungeambiwa maneno matamu haya: “mna thamani mbele yangu, kwa kuwa nimewapa hadhi na kuwapenda.” Haya ni maneno ya Mungu.
Tunafahamu kwamba tuna shida mbalimbali katika maisha yetu. Shida ya uchumi ni rahisi kutambua, na wengi wanapambana kila siku ili wapate hata kidogo tu cha kulisha familia. “Kwa nini Mungu haoni hali hii na kunisaidia kama ananipenda?” Pia tunaweza kuwa na taabu ambayo sio rahisi kwa mwingine kugundua. Tusijidanganye na kusema hatuna shida iliyofichwa. Tunayo. Na wewe unaweza kuona kwamba shida yako inazidi, na inakuwa ngumu kiasi kwamba hujui kinachofuata ni nini. Katika hali hii unaweza kuona kutokujaliwa na Mungu kabisa. - Na kusikia juu ya upendo wake inasababisha tu ukasirike. ”Upendo ndio huo, basi. Haina kitu kwangu”. Tuko katika maada mgumu sana na haina jibu kwa rahisi.
Mwanamke tutakayemkuta leo alikuwa anatafuta upendo, uhuru na amani kama tulivyoongea kipindi kingine, sisi wote tunatafuta mambo haya juu ya mambo yote mengine. Lakini huyu mwanamke pale alipoangalia na kutafuta, hakuweza kuyapata. Labda pia wewe uko kwenye hali ya kutafuta sana upendo, uhuru na amani, lakini baado hujayapata vizuri. Labda unaangalia mahali ambapo haipo!
Dorena Jakobo, "Mama Eliyah", alilelewa katika familia ya kipagani, lakini yeye na dada yake walivutwa na mambo ya kanisani. Na bila wazazi kujua, wakaenda kusali na baadaye wakabatizwa. Lakini hata kama aliokoka wakati wa utoto, Dorena alipokua, alikuja kuishi nyuma ya Neno la Mungu, na kukaa katika ndoa mbaya.
Dorena Jakobo, "Mama Eliyah", ni mtoto mdogo katika familia yake na amekutana na vikwazo vingi maishani, hata hivyo, baba yake mzazi aliokoka kupitia yeye. Sikiliza na utabarikiwa na ushuhuda wa Dorena Jakobo.
Anakuita! Amekuja kukutafuta pale ulipo. Anabishahodi kwako. Si kwa jirani. Kwako. Anataka kuingia. Inaonekana kwamba haondoki mara akiona hakuna jibu. Ana haja kweli, na anaendelea kupiga hodi.
- Mpendwa msikiliaji – Umemsikia? Tega sikio sasa, umsikie leo.