RIZIKI TOLEO LA 1, 2020 'Ujenzi wa Familia Imara'
Cathbert Msemo
Katika toleo hili la RIZIKI tunaangalia mada isemayo, “Ujenzi wa familia imara”. Lengo ni kuibua na kujadili changamoto zilizopo kwenye taasisi hii muhimu ambayo mwanzilishi wake ni Mungu mwenyewe pale bustani ya Edeni. Ni wito wa kuliamsha kanisa na jamii yote, kuwa taasisi hii inapaswa kulindwa, kuimarishwa na kupiganiwa kwa nguvu zote.
Ndani ya toleo hili utakutana na baba mwenye hekima ambaye katika uzee wake alihakikisha kuwa mwanawe mpendwa anapata mke, ambaye ni chaguo la Mungu kwa ajili ya ujenzi wa familia imara.
Pia utapata makala nyingine nyingi kama majukumu ya wanandoa, sababu za talaka, shuhuda na wimbo. Ni imani yangu utabarikiwa na kuimarika katika ujenzi wa familia imara.
Kusoma Riziki Online bure, Bonyeza HAPA