Twende toleo la 4, 2018 linapatikana
Cathbert Msemo
Siku zote tunaona watu wakienda huko na huku kutafuta riziki. Wapo walioajiriwa, wakati wengine wanafanya kazi zao wenyewe, au wanapata nafsi ya kuwa viongozi serikalini au kanisani. Kupitia kazi hizo wanapata ada ya shule, chakula, wanajenga nyumba nzuri na kununua vitu vinginevyo wanavyohitaji.
Wakati watu wazima wakienda kazini, sisi watoto tunaenda shule kusoma. Ndiyo kazi yetu. Pia tunaenda kanisani, na tunapata muda wa kucheza na wenzetu kwa furaha.
Lakini je, umewahi kujiuliza hayo yote yatawezekanaje kama hakuna amani? Amani ni kuwa na hali ya usalama uletao raha ya kufanya kazi zetu na raha moyoni. Kusiwe na woga moyoni mwako, wala ugomvi kati yako na mwingine au vita kati ya nchi na nchi, kwa sababu amani ipo.
Amani yetu sisi Wakristo inatoka wapi? Karibu usome toleo hili ujue zaidi maana ya amani.