Shindano la uandishi wa kitabu kwa vijana
Anne Gihlemoen
“Kujua hekima na adhabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa mated ya busara, kaaika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; mwenye hekima asikie na kuongezwa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.”
Soma Biblia hushiriki katika wito wa kuwaletea vijana habari njema ya Biblia kuhusu Yesu Kristo ili wamwamini na kumfuata. Kwa hiyo tunawakaribisha wote wenye vipawa vya uandishi waandike kitabu kwa vijana wenye umri wa miaka 13-19.
Masharti kwa mswada:
· Lugha iwe ya Kiswahili, na ieleweke kwa walengwa
· Mfumo wa uandishi uwe simulizi au hadithi
· Ukubwa wa kitabu usizidi kurasa 50 zenye maneno 400-500
· Yaliyomo yakidhi malengo yaliyotajwa hapo juu
Ahadi ya Soma Biblia:
· Mswada utakaoshinda utachapwa kama kitabu kwa gharama za Soma Biblia
· Pamoja na heshima ya kuwa mshindi, mwandishi wa kitabu hicho atalipwa mrabaha wa asilimia 10
· Waandishi wengine wote watarudishiwa mswada wao, ukiwa pamoja na maoni machache; hatutautumia kwa namna nyingine isipokuwa kwa idhini ya mwandishi
“Unaweza kufanya chochote kwa kuandika!”
Tuma mswada wako kwa:
Soma Biblia, S.L.P. 2696, Arusha
au
publishingmanager.somabiblia@gmail.com
Tarehe ya mwisho kutuletea mswada ni 31 Machi 2018
“Reading is to the mind what exercise is to the body.”