NDOA YENYE FURAHA
Cathbert Msemo
HATIMAYE KIPO!
Kila anayewashauri wanandoa anajua ni kazi yenye changamoto nyingi. Kwa hiyo ni kazi muhimu sana kuwasaidia wanandoa watarajiwa kuweka msingi imara kabla hawajafunga ndoa. Lakini unajua pia ni kazi kubwa na inachukua muda mwingi – muda ambao pengine huna.
Ndoa Yenye Furaha kimeandaliwa kiwe msaidizi wako. Ni kitabu cha kiada kitakachowaandaa vizuri wanandoa watarajiwa kwa ajili ya kupokea mafundisho ya kichungaji. Mambo ya ndoa yameratibiwa kwenye vipindi sita. Pia kuna mazoezi ya kufanya yatakayowasaidia hao kuelewa na kukumbuka vizuri zaidi mafundisho waliyopitia.
Wachumba wakija kuomba kufunga ndoa kanisani, uwe na Ndoa Yenye Furaha ofisini mwako ili uweze kuwapa nakala na kuwaambia wajiandae kwa kipindi cha kwanza cha mafundisho ya ndoa kwa kusoma sehemu fulani katika kitabu.
Usijinyime furaha ya kuwa na kitabu hiki kama msaidizi wako katika kazi uliyo nayo ya kufundisha mambo ya ndoa. Mwandishi mmoja wa Ndoa Yenye Furaha ni Askofu Blaston Gaville, KKKT Dayosisi ya Iringa, ambaye ana uzoefu mwingi wa kuwafundisha na kuwashauri wanandoa.