ELIMU YA IMANI NA KIKRISTO/CHRISTIAN EDUCATION
Anne Gihlemoen
Hutoa msaada thabiti kwa sisi sote tunaowalea watoto. Upendo pasipo mashartini mbinu ya msingi, lakini pia kukaa pamoja kunakojenga, nidhamuna mbinu nyinginezo zinafafanuliwa kwa makini. Kila atakaye kuwapa watoto wake maisha yaliyo na maendeleo yenye afya, yampasa akisome.
Ni hazina kubwa kwa wote wanaotaka kufahamu ukweli wa Imani ya Kikristo. Kimeandikwa na profesa wa theolojia mwenye fokasi ya Kiinjili na kwa lengo la kumwezesha msomaji kushuhudia, Namjua yeye nimwaminiye! Ni kitabu cha lazima kwa kila aliye na huduma ya kufundisha kanisani.
Je, unatafuta mifano ya kukusaidia kufafanua somo la mahubiri? Jossang alikuwa na kipawa maalumu. Pata mifano 115 yenye umaarufu.
Kinafafanua mtoto anavyotambua tofauti na mtu mzima. Chombo muhimu kwa wazazi na waalimu wote wanaowafundisha watoto imani ya Kikristo.
Kwa njia ya visa 111 vya Biblia, historia ya Mungu na wanadamu inasimuliwa kwa lugha rahisi. Kitabu kinafaa kama ‘Biblia ya wakipaimara’.
Masomo 21 kuhusu imani na maisha ya Kikristo yaliyoandaliwa kipekee kwa ajili ya mafundisho ya Ubatizo kwa watu wazima na Kipaimara.
Je, unataka imani yako iimarike, na maisha yako yampendeze Mungu? Pata mafundisho mepesi na yenye kina wakati mmoja. Kwa vijana pia!
Maswali na majibu 602 juu ya imani na maisha ya Kikristo. Yatakuwa na manufaa kwa watu wengi hasa wanafunzi wa neno la Mungu.
Jifunze jinsi matengenezo ya Kanisa yalivyo na maana hadi sasa.